MAONI YA MNYONGE
Namweshimu fundi seremala kwa meza yake imara
imenifanya niinge ofisini kwa mkwara,
nitakuwa hayawani niki kashifu nyundo yake na kumwambia atumie ya kuni.
kwa mstaarabu fadhila natakiwa nimiminie mambo mema tuyaone siku za usoni.
Waimbaji naomba haya nitakayo sema myape nafasi katika mioyo yenu,
tunapenda kuwaona mki imba kwa order,
sauti ya 1,2,3 na 4 ki kawaida wanamuziki wote hawawezi imba,
wengine wakamate gita wapige kinanda na tumba kuimba kuendelee
sanjari na hilo yale mashairi ya nyimbo zenu mbona hayana vina waungwana
hamjawa kima mtoe sauti zisizo na mpangilio,
kama tungekuwa serious waimbaji wasingeimba nyimbo za msibani harusini
kama mwanadamu nililiyekamilika nataka muziki unikoshe nyoyo na si vinginevyo,
nimechoshwa na tungo zao zisizo na utashi wala weledi
nisicho elewa ni kwanini nyimbo zao hazi ishi kama vibao vya remmy ongala na TX moshi
hapo hakuna ubishi,kwa kawaida mtaka cha uvunguni sharti ainame,
kama tunataka sikia sauti zilizonyooka kama mithili ya mshale,
beti zilizo pangwa kiustadi ziwashangaze wale waliotubeza .
tunatakiwa kuwa mafundi wa kutofautisha mambo.
Waungwana haya ni maisha macho yetu yanatakiwa yaweze kuona mavi ya panya kwenye unga, kutofautisha kunguru na boeng katika anga,
na kumtambua mchezaji na shabiki uwanjani,
waungwana kipindi hiki macho na maskio yetu yatatusaidia kutouziwa mbuzi ndani ya gunia,
sote tunajua kuwa gari letu halina mafuta na limesimama njiani na tunahitaji petroli ya uhakika
iweje tuelekee kisimani inashangaza waungwana hata diesel haifai licha ya kuwa yapo magari yanayoitumia,
kumbukeni enjini yetu sio sufuria maji na chai kuchemshia maana maji yakimwagika hayazoleki
mkono na kijiko vyote vya weza kukushibisha cha msingi chakula kiwe bora.
Comments
Post a Comment