MWANANGU NISIKILIZE.
Mwananguu umekua sasa wajua maneno kuchakata na kukataa wajua tena katakata, tena siku hizi kuna smartphone akilegalega tu unamtia adabu.
Umetimia wasaa wa wewe kwenda miaka 20 imepita wajua nani anakupenda, kwa maumivu uliyoyapitia kwa Yule mtalaka sina shaka na maamuzi yako najua ni ya uhakika wajua yupi lului yupi takataka.
Mwanangu mimi ndio baba na mama nakusihi waangalie kwa makini Juma na Uledi wana maneno hao tena ya weledi, kumbuka kilio cha kweli hakipimwi na wingi wa machozi wengine wanakata vitunguu mwanangu.
Mwizi hapigi hodi, eti leo njaa ni shibe na shibe ni njaa uongo na kata jiwe ni nyama na nyama ni jiwe mwnangu we si nguruwe ule takataka.
Mwanangu kabla hujainngia ndani ya kile chumba na kula kiapo jiulize akikupeleka ludewa je kodi ya meza ipo au mpka ugeuze shingo uanagaze mkopo kama kwa Yule,
Nataka ule vitamu mwanangu kuku, nyama, ugali wa muhogo usahau ukoko, matunda mezani mwili ujae vitamin kipolo weka pembeni,
Naomi asha alex na masalu wanakutegemea ile siku watakapo tia miguu kwako hawatopenda kukuona ukichechemea.
Kidonge cha mwisho mwanangu nakupatia tena meza kwamezamengi yenye chumvi, viluilui, meupe kama sarujihata yele unayo share na mifugo kumbuka gazeti la jana haliuziki si maanishi uache kusoma vitabu vina mambo mema,
Yapuuze yasiyo na uhakika vioja visa ongeza kurasa ule muda unaosubiria umbea wa insta katafute shekel peleka nyumbani msusa.
Comments
Post a Comment