TANZANIA NCHI YANGU
Tangia upate uhuru mwaka 1961 mpaka sasa ni mambo mengi yametokea ambayo ni ya kuigwa na kuachwa mara moja ili kuiweka Tanzania katika nafasi ambayo inatakiwa kuwepo. Kama wale waliotangulia mbele za haki miaka hiyo Tanzania inapata uhuru wangepata nafasi japo kwa sekunde chache kuiona Mwanza, Arusha, Dodoma, na dar es salaam watapigwa na butwaa maana mengi yamefanywa na serikali na wananchi wake katika kuijenga nchi yao kwa kiasi . Sanjari na hilo mengi yamefanya ambayo yamefanya watanzania wanung’ungu’nike na kujutia mara nyingine kuwa waafrika hata kuzaliwa Tanzania.
Katika siasa za nchi yangu chama cha mapinduzi kimekuwa madarakani sasa kwa muda wa takribani miaka hamsini kimekuwa madarakani na kuingoza nchi mpaka sasa mbapo kwa sasa kipo katika juhudi za kuendelea kubaki madarakani, licha ya kuifanya Tanzania shamba la bibi, uchumi kuporomoka kwa aslimia 20%, rasilimali zetu zinawanuafaisha wageni, wanyama pori kutoroshwa kwa wingi. Japo bado kuna matumaini kwa baadhi ya watanzania kwa CCM. Vugu vugu la kisiasa kwa sasa ni kubwa kwani upande wa upinzani wana nguvu ya kiana yake na huenda mabadiliko yaka tokea kwa namna UKAWA wanavyo pambana kushika hatamu za uongozi nchini.
Lakini kama ilivyo ada kwa siasa za kiafrika na hasa nchi masikini, na kwa serikali iliyoko madarakani kuvi=unja mari za demokrassia wanayo iabudu na kutokuwa na utawala bora, huwa haziwezi kuachia hatamu mara nyingi kwakuwa kila nguvu ambayo inaweza wakisha mdarakani iko mikonoini mwao kama vile jeshi, polisi na tume za uchaguzi. Ndio maana kila kukicha tunaona vurugu katika nchi zinazo pata vuguvugu la kisiasa hivi majuzi Burundi watu wamehama makazi na kuuwawa kwa vile raisi wao pierre nkurunzinza hakutaka kaa pembeni na kuacha wengine washike dola. Congo mpaka leo hakuna amani tangia nazaliwa nasikia na kuisoma katika magazeti na vitabu damu inamwagika sana yote hayo ni siasa kutumiwa vibaya.
Kwa Tanzania vyombo vya habari vimekuwa viki hamasisha wananchi wake kupiga kura na kuachana na kuanzisha vurugu na kukubali matokeo ya uchaguzi, lakini kwa upande mwingine hilo ni kiashiria kuwa ile homa na tabia ya chaguzi za Africa inaonekana hata kwa Tanzania na imebidi ikemewe mapema. Kibaya zaidi wanasiasa wanatoa maneno ambayo yanachochea wafuasi wao kuwa na ari ya kuanzisha chokochoko maneno kama’’ pata chimbika’’ hayana nia ya kuwafanya wapiga kura wawe na nia ya kumaliza zoezi la uchaguzi salama.
Nigeria waliishangaza dunia pale walipomaliza uchaguzi wao salama na goodluck jonathani aka achia dola kistaarabu na kidemokrasia, hata wao hawakuwa na imani na kuvuka salama.
Tanzania ina kila sababu ya kumaliza uchaguzi huu salama maana kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa ili tuweze ondokana na janga la umaskini, ujinga, maradhi na rushwa hayo yote hayawezi timizwa kama hatuwezi fanyauchaguzi wa huru na haki.
Mali asili zetu zinatakiwa kutunufaisha wote na kuifanya nchi kunga’ra katika medani za kimaendeleo na kiuchumi, kuna watu ambao wana hitaji kuona tunapiaga wenyewe kwawenyewe ili kujinufaisha kwa kutumia rasilimali zetu na sisi kumwaga damu inayo laani ardhi yetu, mpaka leo congo mitutu ya unduki bado inasikikia lichanya juhudi za kuleta amani.
Mtanzania usitumike kuchoochea vurugu, kuleta shari wala kuvuruga zoezi la uchaguzi maana amani ina thamani na kuipoteza ni jambo rahisi pale usipofikiri kwamakini na kukubali kuwa chambo.
Kama maneno ya watanzania wenzangu yanavyorindima katika vyombo vya habari, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI, WATANZANIA TUVUMILIANE.
MUNGU IBARIKI TANZANZIA.
Comments
Post a Comment