TUKACHAGUE KIATU
Kaka hebu acha kuchati ili twende tukachague kiatu iwe dukani au mnadani maana chacha aniuma kweli nimepekua sana karatu asikwambie mtu, kwa nyakti hizi zile raba zenye rangi za kumete meta sizitaki chagua langu ni safari buti ni sahau kuzungushia nyuzi.
Kaka ilituendane na wakati itabidi tununue viatu pea tatu pea ya kwanza iwe ya kuvaa kuelekea kazini ena inatakiwa kiwe imara maana ndicho kinacho nipa maini. Kaka tusije  ingiwa na upofu wa ghafla na kuchagua sicho tutakuwa kama Yule mama aliyekata mkono wa mwanae kwa kuchezea mavi mkononi wakati amaekuwa akitumia wake wa kushoto chooni mpaka anaingia kaburini.
Ile pea ya pili itakuwa ni ya kuvaliwa wakati wa matembezi maalum maeneo ya kujidai hapo nitakuwa makini maana nisije chagua mdosho ukanitoa nishai.
Siku zote adhabu ya kaburi aijuaye maiti kaka zile pea zilikuwa zinanibana kweli hakuna mfano miguu imeniuma mpaka nikazoea kuikata nisingeweza kutembea bado  nahitaji yaliyopita sindwele tugange yajayo.
Kaka kwa vile mteja ni mfamle hatuhitaji nunua visivyo bora, mathalani pesa ipo hatuna shaka cha msingi bei zao ziwe na mashiko  sisje kula kwetu nina uhakika tukipita katika maduka na minada yote tutakuta kiatu kwa sababu ‘’anaye tafuta hachoki akichoka amepata’’
Kaka wauzaji wamejipannga vilivyo kuhakikisha kuwa hawaingiii hasara wana maneno ya ushawishi yanayokufanya uvutike ili ununue bila ubishi ‘’nunua vyangu nina uhakika utapendeza tena vinanedana na kiapara chako’’ , ‘’ mteja ni change mimi siuzi feki original vimejaa tele jichagulie kiatu kiyabadili maisha yako’’.
Kaka sio kila ulimi unao kutamkakia ‘’karibu tule’’ unania ya dhati ya kuongeza kijiko katika shani ili kusosomola kuendelee
Kaka kama wanafunzi darasa la 5A mwalimu na wanafunzi wakikesha wakisoma ni dhahiri kuwa matokeo yao yatakuwa chanya na mitihani yao itakuwa imesheheni vema, lakini darasa lile lile mwalimu na wanafunzi wakikesha wakokotoa maswali ya mtihani wa kesho ni dhahiri kuwa matokeo yao yatakuwa hasi lakini mitihani yao itakuwa na vema za kumwaga vema midosho.
Kaka pea ya tatu itakuwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kikiwa imara kitanifanya nilale kwa amani ndani kwa jinsi nilivyo makini uchaguzi wangu hautonifanya nijutie yamkini ivushayo nimbovu safari hii niko makii hata kama niko uluguru.
Kaka nashindwa kuelewa malumbano ya wauzaji maana hawapendani na wanayo yafanya ni sawa na kutwanga maji, cha msingi wajipange isawa sawa waniambie kwa ufasaha uimara wa kiatu na maneno yao yasiote mbawa.
Siku za usoni pilka pilika zitakuwa nyingi na viatu lazima vihimili suluba maana ukitaka uzuri sharti udhurike.
Nataka kiatu change kiwe na ngozi ngumu kama ya mamba pole mshonajji kwa yaliyokusibu, soli yake isitoboke kwa kukanyaga miba ukibarikiwa kizazi huna budi kushika mimba, na kamba zake zidariziwe kwa ngozi ya samba zisikatike nitakaposakata rumbakiwe na rangi yeyote, bluu kijani njano kinifikishe makutanno.
Jino la pembe si dawa ya pengo kiatu changu nataka kiwe namba 43

Comments