UKWELI
Ukweli,
Ni sawasawa na chroquine anayopewa mgonjwa wa malaria lawama tuwape mbun na neti cha ajabu haitaki na mhofia siha yake ni ya mashaka na sidhani kama siku yake ya kuzaliwa ataifikia.
Ukweli,
Ni kwamba ile chupa ya uhai thamani yake ni yale mai yaliyomo ndani, yakikata kiu yako huitupilia jalalani sanjari na hilo wenzako huipeleka nyumbani na kuitilia asali wanaokoa mazingira.
Ukweli,
Nauona pale napo kumbuka ‘’ alalaye usimwamshe ukimwamsha utalala wewe’’ juma john masele tujipange paja kuleni shingo yanitosha siwaonei gere, matumaini huniingia pale yale mambakuli ya Ruvuma Dodoma geita manyara mtwara na arusha yaponena ‘’ aibu ya maiti aijuaye mwosha’’
Utanisaidia kutathimini haya niliyo yasikia ndani basi nikija nyumbani’’ bora baba wa kambo taikoa hii familia’’ walisahau yakuwa baba wa kambo si baba labda mambo mengi kichwani na kujua pundamilia wa Serengeti na yule aliye katika lami ni sawa lahasha zile ni alama za barabarani.
Mpendwa amini nayo kwambia maana nimeyashuhudia ukisema yalio kweli yatakuweka huru, giza litamezwa na nuru.
Geografia nimeisomea mwalimu marifa kichwani ameniwekea na kudurusu nimedurusu ndio maana nina kwambia mvua yaweza nyesha jangwani
Ni Ukweli,
Usipingika kuwa  ubongo ndio uliowaza na kutengeneza AK 47& BARETTA, pia uliwaza na kuwazua na kuleta majaketi yasiyo penyeza risasi, inanipa ahueni na matumaini ngoja nisubirie lile basi linipeleke misasi.
Ukweli
Kile kinyesi wenzako walichokipisha njia na kupita pembeni hwakuwa wajinga naamin hawatokubeza ukiwaiga,
Moyo wanikimbia pale taswira yaw ewe kutaka kukiruka nahofia waweza anguka na kukilalia, maana wanajua ukweli kuwa vita vya panzi furaha ya kunguru.

Comments