Safari Imeanza.
Mwaka
jana niliomba nauli nilitoa kauli safi yenye kumfanya dereva mashuhuri
asiniache stendi ya basi. Honi nyingi zilisikika wapiga debe nao walimiminika
‘’mama njoo upande gari liko wazi masaki mikocheni mbezi ingia gari iko wazi,
ingia usiende kule wezi wakutoe
machozi’’.
Wazee
walinena yakuwa miruzi mingi humpoteza mbwa hatari zaidi pale miruzi inapomuita
ikimwonesha nofu kubwa zaidi ya kichwa chake . ninajua mnapenda waita mbwa wenu
majina kama samba!, chui! Hata tiger!majina haya hayana maana kama utashindwa
mfundisha mbwa wako tofauti ya mluzi wako na wa kibaka pale unapomuita samba!
Hata Yule Chloe wa jirani apate kuiga.
Kaka
safari imeanza abiria wameona mwendo wa dereva na wameona anavyotii sheria bila
shuruti kweli uendeshaji anauweza, mpaka sasa tochi hazijamweka hatiani kwani
kwake ni kama alama za barabarani kwani aepukaye uovu si mpumbavu. kaka kipindu
dereva wetu anachaguliwa kushika usukani baadhi ya mafundi rejeta hawakumkubali
‘’ kaghushi leseni” walinena, safari ya leo mwaka jana tochi zilimulika kama
jua faini zikamwagika nani aliyejua ustadi wa dereva wa leo sote tunafaidika.
Aliyekando
haangukiwi na mti abiria 45 si mchezo ni roho za watu, kondatka wetu namwona yu
makini si type ya kuyumbishwa na wapiga debe hakuna kucheza rede kazini. Maiti
haiogopi kuoza wote tunaelekea sehemu moja safari itakuwa ya fanaka tukiombeana
ukisika Guuuu! Mwambie tingi angalie mizigo.
Wengine
nimesikia kelele zao viti vya nyuma ‘’nguvu ya coca-cola mafundo saba imekwisha
chupa kavu’’wapendwa abiria wenzangu tuwe wavumilivu sito shangaa kumwona chura
kikaangoni niki izuru Beijing lakini sitegemei mwona masanja akikaangiwa kiepe
wakati ana unga tena wa udaga ndani kwake wansafari bibi mzuri hakosi kilema au
mmesahau ajali za mwaka jana siwatishi Tunakumbushana.
Kaka
nina enjoy kuona miti inavyopishana na mwendo wa basi kiti change cha dirishani
kina nipa amani. Ninamatumaini ya
kutofaulishwa maana bendera hufuata upepo ninayoiona sasa ni ya chuma. Sina cha
kusema zaidi ya kumkumbusha dereva jap ndo umeingia gia ya kwanza na mlima
unaufuata abiria wako tutakuwa sikio lako la tatu tairi litakapo pasuka maana
cheo ni dhamana.
Kaka
niko safarini neno la mwisho pale unapohitajika mchinja ng'ombe njiani sitegemei
kuona kadi ya BVR. Tuombeane uzima si kazi ndogo kubadili gogo kuwa kiti.
Padili
16.
Comments
Post a Comment