TUIOMBEE BURUNDI
Nakumbuka katika mifano ambayo nilikuwa nikiitoa katika
mitihani na hasa mitihani ya historia na uraia ilikuwa ni kuhusu namna gani
nchi za afrika zinavyo mezwa na machafuko yanayosababishwa na siasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe, katika maandishi ya
mwalimu wangu nakumbuka mpaka leo Jina la nchi ya afrika mashariki Burundi
lilikuwa kati ya majina ya nchi yanayotajwa kuwa ni mifano ya nchi zenye vita,
na machafuko ya kisiasa. Burundi ni moja
kati ya nchi masikini zaidi afrika na duniani kwa ujumla, watu wake wanaishi
katika mazingira mabaya ya umasikini, machafuko ya vita yaliodumu kwa zaidi ya
miaka 20 yameiharibu Burundi. Tokea mwaka 1993 mpaka 2006 watu wanauwawa na
damu inamwangika tena damu inamwagika ya wasio na hatia wakiwawengi wanawake na
watoto, mauaji ambayo yanachochewa na ukabila. Wa hutu na watutsi ambao
wameshindwa kupendana na kuishi pamoja, chochoko zinaibukana na uvumilivu
ukawashinda na kupigana jambo lilioichafua Burundi mpaka leo. Nchi hiyo ambayo
imezungukwa na ardhi pande zote bila maji(nikimaanisha bahari na maziwa)
inategemea vyanzo vya nchi jirani kuendelea mfano mzuri ni bandari ya Dar es
salaam inayopakua mizigo mbalimbali inayosafirishwa kwenda Burundi . Leo hii
takribani watu 400 wameuwawa kwa machafuko ya kisiasa yale yale kama
yaliyotokea miaka iliyopita hata kabla sijajua, kuandika vyema, haya yote ni
sababu ya rais Pierre Nkurunzinza kukataa achia wadhifa alioshikilia kwa mihula
miwili.
Kutokuheshimu katiba ya nchi yake, na kutumia
madaraka vibaya pierre nkurunzinza amefanya jambo ambalo watu wa nchi yake
wanateseka hasahasa kina mama na watoto. Kiukweli hapakuwa na haja ya yeye
kuendelea hodhi madaraka kwa muhula mwingine wa tatu, licha ya katiba inayo
mwongoza kutokuwa na utaratibu wa namna hiyo. Kwa tafsiri ya haraka inaonyesha
kuwa amesha sahau yalioikumba nchi anayoiongoza maana ni 2006 tu nchi ikaanza
tulia. Nina jaribu tafakari ni aina gani ya washauri alionano maana nadhani
hawakufanya kazi nzuri, nina uhakika walikuwepo na kwa mazingira ya nafasi
aliyonanyo ni watu werevu na wenye ustadi wa kunyambua na wanaoaminika walikuwa
sambamba nae. Iweje leo raia takribani 200,000 watafute hifadhi nchi ya jirani
Tanzania, licha ya kuwa nchi mama yao ina ardhi ya kuwalea lakini kwa ukatili
wa mtu mmoja leo hii hawana tena amani, ile historia ya nyuma imerudi na
kuitafuna nchi yao, na kuwabatiza majina mapya, ‘’ WAKIMBIZI’’.
Nina andika ukurasa huu nikiwa na masikitiko sana,
nina waza maneno ya Tony Blair aliyoyatoa mwaka 2001 kuwa afika ni kovu katika
dhamiri yetu, akasisitiza ya kuwa dunia kama jumuiya inatakiwa kuiangalia afrika na kuiponyesha
maana isipofanya hivyo, afrika itakuwa imezama katika maovu na kuwa na hasira.
Haya maneno yananifanya kuona namna gani nchi za magharibi zinavyoiona afrika,
zinaona afrika kama janga, gonjwa hatari la kuambukiza ambalo linatakiwa
kutibiwa mapema, maana uvunjifu wa katiba kufaidisha waliojuu, unaonekana kwa
dhahiri bila woga ndani ya nchi za kiafrika na unasababisha maafa makubwa kama
yanayotokea leo Burundi. Kila kukicha milio ya risasi, na miili kuonekana ovyo
mitaani ikiwa na matundu ya risasi kichwani. Hii ina maanisha nini kuna kikundi
cha watu kinafanya haya kinalenga watu, kwa uelewa wangu wa mambo ya kijasusi, kupigwa
risasi ya kichwa ni ishara ya kuua kwa uhakika bila kuwa na mashaka ya mpigwaji
kupona. Na hii inaonesha ya kuwa mauaji haya yanalenga watu. Jaribio la
kupinduliwa Nkurunzinza liliposhindwa liliashiria kuwa kuna viongozi wa juu wa
kijeshi hawamuungi mkono rais na ni wasaliti nadhani hilo lilimkasirisha sana
Nkurunzinza na kufanya uapisho mapema bila kutangazwa hata uchaguzi kuwa wa
mashaka mashaka.
Jumuiya za afrika, hasahasa afrika mashariki
zinatakiwa kuangalia suala hili kwa umakini kubwa sana maana idadi kubwa ya
wakimbizi inazinyemelea nchi jirani na Burundi na Tanzania ambazo ziko karibu,
mzigo mkubwa unazielemea kuwahudimia wakimbizi hao, licha ha hilo afrika
imefika wakati ipumizike na majanga ya kuletwa na sisi, miaka iliyoipita
imetosha kwa vifo vya watu kwa maelfu, sasa ni wakati wa kujipanga na kuleta
maendeleo, kwa haya yanayotokea Burundi ni ishara ya kurudia makosa makubwa
ambayo yanamaumivu makali sana.
Naisihi jumuiya ya Umoja wa Afrika kuiokoa Burundi
na vita, kuokoa maisha ya watu yanayozidi potea kila kukicha, kuvamiwa kwa
kituo cha kijeshi kuanashiria kuwa kuwa kikundi cha watu wasio na hofu na
dhamira yao ni kuangamiza, polisi na jeshi hawawezi tuliza machafuko kwa nguvu
zao sio kwa namna ambavyo jamii inawachukulia hasahasa waandamanaji. Hebu
waafrika werevu waweke akili zao pamoja na kuikoa Burundi, ifike siku tuyaache
haya katika vitabu vya historia tusivyo taka
vifunua kwa kizazi kilichopita.
Mungu Ibariki Afrika. Mungu Iokoe Burundi.
Comments
Post a Comment