SITAKI SUMU TENA

Sikutaka kabisa kuangalia wakaniambia" fumbua macho taswira yake sio ya kama kichwani kwako", wakanishawishi na kuwahadaa pigeni kwa wingi picha mnato, pilipili haiwashi daima, itilie ndani ya mchuzi wa sato utamu wa leo si wa kesho .

Batili imekuwa baraka, nyaraka za siri ziko nje kama talaka, sina stara tena tunu zangu ndo wanazozitaka, hawaoni haja ya kukinga maji ya mvua, kazi yao ni kusubiri maji ya bomba kila mwaka.

Tumieni walau akili kidogo tangu lini kichwa kilicho unda meli ya kubeba mizigo, watu hata punda, kiseme" hata sarafu yaweza elea kama Titanic , huenda itavuka mabara kama mkiomba," ninaona bora kurudi zama za kale kutumia maji na jiwe kujiremba, karne hii vioo vya jamii vyanitenda kama solemba.

Siku hizi hakuna tena haya, kukuonesha akiba ya mwenzangu ruksa, uvumilivu haupo na kuacha maembe mabichi yaive ni nadra sasa. Nasikia hatupandi tena miti ya vivuli kwavile embe huwa tamu unaposhushia na umbea wa insta.

Chujio halito baki kutimiza azma ya mpishi, maana nayo yaona katika talakilishi yamenikifu bila ubishi, utu wetu jalala: karatasi, vyupa, na maganda ya ndizi tutupiwe sisi. Si mnapenda kuitwa mabingwa wakati hamtii amri, kufanyika gaga si kupona donda, fanyeni utaratibu wa kumpa salome achambue hizo karanga, mkumbusheni tunu zake asiziweke rehani na protini muhimu kwa afya kuilinda.


Rafiki bakuli na chupa ya maji vyote hukata kiu, lakini kipindupindu kitakuhusu vimelea wakihusika unaisikia mbiu.

Comments