TELEZA DHIDI YA SERENGETI: PALE HISIA ZINAPO SHINDANA NA HOJA


Takwimu za sensa, zinaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya jumla ya watu waishio Tanzania ni wanawake. Toka kuanzishwa kwake, mwaka 1961  wanawake wa Tanzania,w amekuwa na mchango mkubwa katika uchumi, siasa na elimu, hil halina shaka. 

Vivyo hivyo, katika anga za kimataifa, Utalii umekuwa ukitupa nafasi kubwa ya kujitanua na kujitangaza, hasa kwa vivutio vyetu ikiwemo Serengeti-yenye Zaidi ya KM za mraba 30,000, moja katika ya maajabu saba ya dunia, papo hapo imetupa heshima kushinda tuzo ya hifadhi bora barani Afrika(2019). Kina-mama na utajiri wa asili vyote ni tunu zetu, abadani hakuna wa kubeza thamani yao, lakini kwanini tuna vishusha thamani kiasi hiki kwa kusukuma agenda zisizo na msingi?

Siku kadhaa nyuma, kumekuwa na mirindimo ya kashfa, kubeza, kusimanga kwa watu: walio ona habari za Serengeti na ushindi wake kuwa njema machoni/masikio pao kushinda habari chafu za “Teleza” na vitendo vyao, kuitwa na makundi ya watu mbalimbali kuwa ni watu wasio ona huruma kwa kina-mama huko mkoani Kigoma, wanaopitia gathabu ya wanaume wabakaji wanaoitwa “Teleza”. Sababu ya kwanini wanaitwa jina hilo sihitaji kusema, inasikitisha kueneza habari zao za laana, ila kwa umuhimu wa Makala hii ni tija kueleza na kulaani matendo yao.

Tabia zao zenye kuleta hofu mioyoni mwa watu wote: wanaume na wanawake, zimeanza rindima toka mwaka 2016, ambapo  vyombo vyetu vya habari vilitupa undani wake, ambapo wamejeruhi wanawake, kwa kuwacharanga mapanga pale walipo jaribu kupambana, kulinda utu wao, Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kime repoti kwa kina juu ya matukio haya na kulaani vitendo hivi visivyo vya kiungwana na vinavyo ogofya jamii zetu.

Mwaka, huu kesi kadhaa zimeibuka mkoani Kigoma, zinazo husisha vitendo hivyo hivyo, LHRC imeonyesha takribani matukio zaidi ya 40 ambayo yametukia ndani ya mkoa kwa mwaka huu. Jeshi la polisi kama ilivyo ada, limejikita kuhakikisha watu hawa wanakamatwa na kutiwa nguvuni, kuweka usalama na utulivu kwa wananchi.

Vyombo vya habari vimetumia nafasi yake ya kuwapa-wananchi-taarifa yakinifu juu ya matukio haya. Ni jukumu la waandishi wa habari kufuata miiko na kanuni za uandishi bora kuhakikisha mizani ya usambazaji habari imefuata vyema. Lakini, utata umeibuka pale Rais wa Tanzania, Dr. John Joseph Pombe Magufuli, alipo toa duku duku lake, narudia duku duku lake juu ya vyombo vya habari kuto ipa habari ya Ushindi wa Hifadhi ya Serengeti nafasi moja kwa siku moja katika vichwa vikuu vya habari, katika magazeti yake.

Nipende, kuwa fahamisha (kwa wale ambao hawajapata pitia hili) yakuwa katika uandishi wa habari yeyote kuna vitu muhimu kwa kufuata ikiwemo, umihimu, ukaribu-wa-habari- na-wasomaji, muda na matokeo ya habari yenyewe. Kama, mwandishi wa habari kijana, niliona habari ya Serengeti kukidhi vigezo KABISA bila shaka yeyote, vivyo hivyo habari ya kinara wa ubakaji “Teleza” huko Kigoma, inakidhi vigezo vyote,pia.

Cha kushangaza, maneno ya Rais yamegeuzwa na kuweka katika mizani isiyo sawa, na wengine kuingia katika mtego wa kujenga hoja uitwao kwa lugha ya kigeni “ Strawman Fallacy” , mtego huo unaonesha namna watu wanavyo weza tumia hoja yako kinyume na matakwa/nia ya maneno yako na kupindisha uhalisia wa mambo katika hoja wanazo taka ziwe.

Katika Mitandao ya kijamii hasa Twitter, kurasa yangu, ilisheheni, maoni ya watu waliokuwa wakisema ya kwamba, ushindi wa Serengeti hauna mashiko kwa wananchi wa kawaida maana , hawaendi katika mbuga hizo, wengine wakidiriki kusema hakuna utu sasa pale tunapo shadidia tuzo na si kutetea wanawake wahanga.

Yote hayo juu, ni mlundikano wa hisia tupu na si hoja. Nipende kusema ya kwamba, maneno ya kiongozi wa taifa yalichukuliwa katika muktadha na maana tofauti kabisa, nina amini ya kwamba hakuwa na nia ya kudharau wala kukebehi vitendo vya hao mafedhuli wasio na haya kwa wanawake, ila nina amini, kama mtanzania, alitamani kuona Tanzania, walau kwa masaa 24 ikisomeka vyema katika vichwa vikubwa vya habari kwenye magazeti kupitia tunu yake Hodari SERENGETI, na habari ya mhalifu huyo kupewa pia nafasi yake lakini katika vichwa vidogo, na si kutokuchapishwa kabisa.

Hoja ilikuwa tuchague, kuendeleza anika aibu ya nchi yetu ama, kwa namna moja au nyingine ipa “SHAVU” Tanzania katika duru za kimataifa na kuzidi ongeza watalii Zaidi na fedha za kigeni, kutanua sekta ya utalii itakayo leta ajira Zaidi na fursa zingine za kibiashara.

Ilikuwa ni kuchagua, kuendelea kuzungumzia maumivu (ambayo ni lazima kwa wananchi kujulishwa) katika vichwa vya habari ama kuitangazia dunia juu ya utajiri tulionao, maana ilikuwa ni nafasi moja tu na haitojirudia tena KAMWE.

Kama ilivyo ada uwezo wa kunyambua na kuya angalia mambo kwa jicho pevu umeonekana wazi katika hili, kuwa dhaifu. Ni muhimu kuangazia tasfiri na kuyachambua maneno katika muktadha husika na kuhakikisha hoja zinazo jengwa zinawekwa katika mizani imara yenye kushibisha azma ya kuanika madhaifu na kuinua mema.

Hebu basi japo mara moja kwa mwaka, tumpe MAMA TANZANIA heshima yake ya kimataifa pale anapo tupa baraka zake, ni hilo tu.


Comments